SMS NA MESEJI YA UPENDO KWA YULE UMPENDAYE. MAHABA PRO MAX 😍😉.

 

SMS NA MESEJI YA UPENDO KWA YULE UMPENDAYE. MAHABA PRO MAX 😍😉.



Tone la mvua huonekana dogo sana, lakini kwa mwenye kiu hulisubiri kwa hamu kubwa. Sms ni kitu kidogo, lakini huonyesha mahali fulani yupo mtu ANAYEKUPENDA, ANAKUKUMBUKA, ANAKUOMBEA, ANAKUJALI na, ANAKUTAKIA mafanikio mema

Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jembe la KUSAMEHE, iwekee mbolea ya AMANI, ipige dawa ya NENO LA MUNGU, itakayoua wadudu wote waharibifu kama ubinafsi, chuki, wivu, dharau, unafki, kiburi, choyo, tamaa na fitna kwenye mmea huu, MMEA HUU (UPENDO) UENDELEE KUWA MCHE BORA KULIKO YOTE KTK MAISHA YAKO SIKU ZOTE

Usimpende mtu tuu kwa sababu uko mpweke, Au kwa sababu ana pesa, kwa sababu upendo Sio pesa wala siluhisho la matakwa yako.

Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia. Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana.

Nakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa,wengi watakuambia maneno kila kukicha,lakini nakuambia wapo ambao kwa hakika watakaokuwa wamelenga kutia doa ndoa yako, rafiki yangu kipenzi kwani wengi waitamani ndoa lakini hawajapata wa kuwaowa

UPENDO ni ubeti wa maneno yaliyo tamkwa mpaka sasa hajulikan nani alietunga!
PENZI ni hadithi iliyocmuliwa lakin mpaka sasa hafahamik nan muhucka, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika muda wote huhis anasalitiwa.

PENZI Ni kama jengo lilokosa nguzo muda wowote unahic litadondoka… Ucnielewe vibaya ckukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wap UMEPENDA au UMEPENDWA! Je eti nikweli kumpenda asie kupenda ni sawa na kusubiri boti airport?

Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.

Mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa unaempenda.

“Watu tumeumbwa Kupendana. Vitu Vimetengenezwa Kutumiwa. Sababu inayopelekea mambo kuwa magumu ni kwamba,watu wanapenda vitu, na kutumia watu.”

“Tumepewa Mikono Miwili, Macho Mawili, Figo Mbili, Miguu Miwili. Ila Kwanini tumepewa Moyo Mmoja..?”

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA❤️ KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO❤️

Maneno mazuri ya Usiku mwema

SMS ZA MAPENZI ZENYE UJUMBE MTAMU KWA MPENZI WAKO