SMS ZA MAPENZI KWA MTU UNAEMPENDA.

 



Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako ?

Najua kuna vishawishi vingi sana uko ulipo, lakini nikiwa moyoni mwako, siku hii itakuwa nzuri zaidi kwetu, upendane daima lahazizi…

Uzuri wako hung’ara kuendana na matendo yako, Ushupavu, upole, ujasiri na uchambuzi wa kweli, kwa yote yajayo mbeleni mwako.

Mapenzi ni nini? Wale wasiopenda huita majukumu, wale wanaoyachezea huita mchezo, wale wasiokuwa nayo huita ndoto, na wale wanaoelewa huyaita mwisho wa safari, na mimi, mwisho wangu ni wewe.

Kulikuwa na vipepeo wawili waliokuwa wanapendana sana, siku 1 waliamua kucheza mchezo wa mahaba. Waliweka ua na walipanga kesho ambaye atakuja mapema na kukaa juu ya UA, atakuwa anampenda mwenzake zaidi. Asubuhi kipepeo dume alienda mapema sana na kukaa juu ya UA. Masikini kumbe jike alifika tangu jana kumwonesha mpenzi wake ni jinsi gani anavyompenda…!!

Jee…!! wewe, utamuonesha nini umpendaye ili aone ni kiac gani..?

Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.

Macho huona na moyo hurdhia,ila co kila kitu jicho lionalo moyo hurdhia.lakn pind moyo urdhiapo upendo moyon huingia.moyo huwa kpofu japo wng wa hisia.upendo ndan ya moyo haupimwi kwa mizani kwa unayemzimikia. moyo wangu umepata hisia Kwa flan licha bdo cjamjua.

Kuna Michezo Mingi hapa Duniani lakini kunawapuuzi wameamua Kuchezea Mioyo ya Wengine na Kuiumiza. Kama Ukimpenda Maanisha.

Moyo upendao kwa dhati. Haujalishi ni kababu au chapat. Ni wingi wa upendo wenye tarakimu kama somo la hisabati. kumpata akupandae kwa dhati pia hyo ni bahati. nimfikiriaye kwa sasa nahc anaupendo wa dhati. Nitashukuru anikaribishe naye nimuonyeshe upendo wa dhat. Huu ni ukaribisho wa penzi la dhati. Wenye wing wa furaha na Lenye pendo la kitanashati

Je unakubali au unakataa kwa mujibu wa sheria ya mahakama ya mapenzi kifungu cha mahaba unahukumiwa kuwa na mimi milele,unaweza kukata rufaa kama hujatendewa haki.sawa?

Naomba upokee zawadi hii ya kiwembe. Amini ndicho kilichotumika kufanyia operation kwa kupasuliwa moyo wangu, kwa sababu nimeoza kwa ajili yako, nimeambiwa ili nipone maradhi haya nipate:- (1)Ushirikiano wako (2)Furaha yako, (3)Upendo wako, (3)Tabasam lako.
Je! uko tayari kuokoa maisha yangu?

Pindi nikukumbukapo chozi langu huwa linatoka bila sababu,kasi Ya mapigo ya moyo Huongezea Pasipo Sababu,nimegundua Nakuhtaji Naomba Unikubalie.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA❤️ KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO❤️

Maneno mazuri ya Usiku mwema

SMS ZA MAPENZI ZENYE UJUMBE MTAMU KWA MPENZI WAKO